Rais Muhammadu Buhari amekuwa mjini London, Uingereza, tangu tarehe 7 mwezi Mei, na baadhi ya Wanigeria walikuwa wameanza kumtaka arejee kazini au ajiuzulu.
Buhari aliondoka Nigeria mnamo mwezi Julai mwaka huu ili kupata matibabu mjini London, ambako alikaa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kurudi nnyumbani mnamo mwezi Machi.
Lakini aliondoka tena mapema mwezi Mei. Wakati akiwa nje ya nchi, Buhari alikabidhi baadhi ya mamlaka ya uongozi kwa makamu wake, Yemi Osinbajo. Taarifa iliyotangaza kurejea kwa rais huyo ilisema kuwa atahutubia Wanigeria kupitia matangazo ya moja kwa moja Jumatatu asubuhi.