Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 23:52

Brunei na Sudan zawekwa daraja la tatu na Marekani kwa usafirishaji haramu


Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeziweka Brunei na Sudan katika daraja la tatu kwenye ripoti ya kila mwaka ya Usafirishaji Haramu wa Watu (TIP) iliyotolewa Jumatatu, ambayo inaweza kuziwekea nchi hizo vikwazo au kupunguziwa misaada na Marekani.

Marekani inazichukulia nchi zilizo kwenye daraja la tatu kuwa haziwajibiki vya kutosha kuchukua hatua dhidi ya ulanguzi wa binadamu na hazifuati Sheria ya Marekani ya Kulinda Waathirika wa Usafirishaji Haramu wa 2000 (TVPA).

“Duniani kote, inakadiriwa watu milioni 27 wanatumikishwa kwenye biashara ya ngono,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika ujumbe kuhusu ripoti hiyo.

“Kwa kutumia nguvu, ulaghai, na kulazimisha, watu pia wanatumikiswa katika mashamba, viwanda, migahawa na makazi.” Brunei inaripotiwa haijamuweka hatiani mlanguzi yoyote kwa miaka saba.

Forum

XS
SM
MD
LG