Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:51

Brazil yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kufariki kwa Pele


People mourn the death of Brazilian soccer legend Pele, in Santos
People mourn the death of Brazilian soccer legend Pele, in Santos

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Brazil uwanja ambao nguli wa soka wa Brazil Pelé alicheza baadhi ya mechi bora zaidi za maisha yake pia utatumika kwa  watu kutoa heshima zao za mwisho siku ya Jumatatu na Jumanne.

Mji wa Santos ambao Pele alicheza huko katika klabu ya Santos umetangaza siku siku 7 za maombolezo katika taarifa kwa umma klabu yake ya zamani imesema heshima za mwisho zitatolewa kwenye Uwanja wa Vila Belmiro, nje ya Sao Paulo.

Pele mchezaji wa aina yake katika soka alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi.

Pia alikuwa anapata ugumu wa kutembea bila kusaidiwa tangu kufanyiwa upasuaji wa nyonga mwaka 2012. Mnamo Februari 2020, usiku wa kuamkia janga la virusi vya corona, mwanawe Edinho alisema hali ya Pele kudhoofika ilimfanya awe na huzuni.

Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.

Gwiji huyo wa Brazil, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Edson Arantes do Nascimento, aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia mwaka wa 1958, 1962 na 1970 na anabakia kuwa kinara wa ufungaji wa timu ya taifa akiwa amefunga mabao 77 katika mechi 92.

Nyota wa sasa wa Brazil, Neymar, alifikisha magoli hayo kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar, akifunga bao lake la 77 katika michezo 124.

Pele alikuwa mfungaji mdogo zaidi wa Kombe la Dunia mwaka 1958 alipofunga bao dhidi ya Wales akiwa na umri wa miaka 17 tu mashindano hayo yalipofanyika Stockholm, Sweden. Rekodi yake bado ipo, na hadi sasa, bado ndiye mchezaji pekee chini ya miaka 18 kufunga bao katika Kombe la Dunia.

Mabao mawili ya Pele kwenye mechi ya fainali yaliisaidia Brazil kutwaa ubingwa wa mwaka 1958, na aliiongoza timu yake kutwaa mataji mengine mawili ya Kombe la Dunia mwaka wa 1962 na 1970.

Akiwa na taaluma ya kimataifa iliyojumuisha mabao 77 katika mechi 92 Pele alitajwa kuwa mchezaji mwenza wa FIFA wa karne ya 20, pamoja na Diego Maradona wa Argentina.

Mnamo mwaka 1975, Pele alijiunga na New York Cosmos ya Ligi ya Soka ya Amerika Kaskazini na kucheza misimu mitatu. Mwaka 2015, Pele alitafakari maisha yake juu ya mchezo huo.

Mabao 1,281 ya Pele katika michezo 1,366, kama ilivyoorodheshwa na tovuti ya FIFA, yalikuja kwa kiwango cha kushangaza cha 0.94 kwa kila mechi. Baadhi ya hizo zilikuwa za kirafiki au alikuja katika michezo iliyochezwa kama sehemu ya utumishi wake wa kijeshi, lakini alikuwa mahiri katika mashindano rasmi, akiwa na mabao 757 katika michezo 812.

XS
SM
MD
LG