Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:49

Bobi Wine aripotiwa kuwekwa mbaroni kwa muda Uganda


Bobi Wine (katika gari ) akiwasalimia wafuasi wake wakati akielekea kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais Kampala, Uganda, Nov. 03, 2020.
Bobi Wine (katika gari ) akiwasalimia wafuasi wake wakati akielekea kuteuliwa rasmi kuwa mgombea urais Kampala, Uganda, Nov. 03, 2020.

Wagombea wa upinzani nchini Uganda waliojiandikisha katika uchaguzi wa rais mwaka 2021, Jumanne wameshuhudia majeshi ya usalama wakimtia mbaroni kwa muda mwanamuziki ambaye amegeukia siasa Bobi Wine.

Wine alichukuliwa kiasi cha dakika chache baada ya kujiandikisha kuwa atatoa changamoto kali kwa Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwepo madarakani kwa takriban miaka 34.

Hamasa, shamra shamra na vigelegele, na uwepo wa vikosi vya usalama vilikuwepo wakati mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine alipojiandikisha rasmi kuwania urais wa nchi.

Wine aliingia ndani ya gari ya Jumanne asubuhi, akielekea tume ya taifa ya uchaguzi mjini Kampala.

Mamlaka ilimpa maelekezo ya kutumia njia maalum yeye kuelekea na hivyo kusindikizwa na magari matano ya polisi, piki piki nne za polisi, magari mawili ya kijeshi na gari moja ndogo ya polisi aina ya Subari, ili kuhakikisha habadili njia.

Kwenye barabara hiyo, kulikuwa na umati wa watu waliokusanyika wakimshangilia. Kuna wakati mmoja, umati wa polisi uliongezeka, ndipo polisi walipotumia gesi ya kutoa machozi ndani ya gari ambayo Wine alikuwa amepanda yeye pamoja na mke wake.

Akiwa anahema kwa nguvu, Wine alizungumza na VOA, “ndiyo, tunasonga mbele, tunajaribu kufika kwenye kituo cha uteuzi, lakini kila mara polisi wanatusimamisha.”

Wine alifanikiwa kufika katika kituo cha polisi na baadaye kukubaliwa kuwania urais na mwenyekiti wa Tume ya Taia ya Uchaguzi, Simon Byabakama na kumsihi Wine kujiepusha na kuwapungia wafuasi wake akiwa ndani ya gari lake.

“Maandamano ya barabarani yamepigwa marufuku. Pili, kama mgombea, tunatarajia utachukua jukumu binafsi kwa wafuasi wako, pamoja na wewe mwenyewe kwa kujiweka kando na mikusanyiko mikubwa na watu,” mwenyekiti wa tume alimueleza.

Katika hotuba yake ya kupitishwa na tume kuwania urais, Wine alimtaja Rais Yoweri Museveni akisema wakati wa kuacha kulalama umefika na kuchukua hatua dhidi ya kile alichokiiita ukosefu wa haki, kutokhofia kushtakiwa na ukandamizaji katika nchi.

“Bwana Museveni, kwa vile umeshindwa kudhibiti uroho na uchu wa madaraka, kizazi chetu kina azma ya kukuokoa katika hilo na kusitisha uongozi wako wa kidikteta wa miaka 35. Katika uchaguzi huu, ninawawakilisha wanyonge, ninawawakilisha maskini, nina wawakilisha hohe hahe. Ninawawakilisha wale ambao wameenguliwa katika mfumo ambao unafanya kazi kwa ajili ya watu wachache tu,” amesema Wine.

Akiwa njiani kuelekea nyumbani, Wine alitolewa ndani ya gari yake na kuingizwa katika gari la polisi na kupelekwa sehemu ambayo haijulikani mpaka baadaye ndipo aliporejeshwa nyumbani kwake. Gesi ya kutoa machozi ilitumika kuwatawanya watu.

.

XS
SM
MD
LG