Blinken alikuwa akizungumza na waandishi wa habari nchini Afrika kusini, ambapo alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini Naledi Pandor, katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika, ambapo pia atatembelea Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda.
Amesema kwamba endapo ulimwengu utaruhusu nchi zenye nguvu duniani kuvamia nchi ndogo itakuwa jambo la kawaida kwa nchi nyingine kufanya hivyo sio tu Ulaya bali kote duniani, bila kuwajibishwa.
Blinken amesema kwamba Marekani inatambua kwamba ni muhimu kuiwajibisha Russia kutokana na uvamizi kwake Ukraine kwa sababu uvamizi huo unatishia misingi ya hali kote duniani.
Russia ilivamia Ukraine Februari tarehe 24 katika kile inakitaka kama operesheni maalum ya kijeshi ili kuwalinda watu wanaozungumza kirusi nchini Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini amesema kwamba hakuna mtu yeyote anaunga mkono vita vinavyoendelea Ukraine lakini mifumo ya sheria ya kimataifa inaonekana kutekelezwa kwa upendeleo, akitaka hatua kama hizo kuchukuliwa ili kuangazia yanayoendelea Palestina