Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:42

Blinken asema Netanyahu amekubali pendekezo la Marekani kwa Gaza


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, akiwa Tel Aviv, mwishoni mwa Jumatatu amesema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameafiki pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano Gaza, sasa inasubiriwa Hamas kukubali.

Wakati huo huo, kampeni ya chanjo ya polio inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa Agosti mpaka Septemba, bila kujali matokeo ya mazungumzo ya karibuni ya kusitisha mapigano.

“Sasa ni wajibu kwa Hamas kufanya hivyo, chini ya usaidizi wa wapatanishi Misri, Qatar na Marekani, kuja pamoja na kukamilisha mchakato,” waziri Blinken aliwaambia waandishi wa habari, bila kusema kama wasiwasi ulioelezwa na wanamgambo wa Hamas umeshughulikiwa.

Ziara ya tisa ya Blinken Mashariki ya Kati toka vita vya Gaza kuanza Oktoba 2023 imefanyika wakati Marekani, Misri na Qatar zikijaribu kukamilisha makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka kati ya Israel na Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG