Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:46

Blinken asema ana wasi wasi kuhusu ripoti ya Rwanda kusaidia waasi


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba Katika Mkutano wa Wanahabari .August 1, 2022. REUTERS/David 'Dee' Delgado.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba Katika Mkutano wa Wanahabari .August 1, 2022. REUTERS/David 'Dee' Delgado.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano ana wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa inayosema Rwanda inawaunga mkono waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano ana wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa inayosema Rwanda inawaunga mkono waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akihitimisha ziara ya siku mbili huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano, Waziri Blinken alisema amesikitishwa na ripoti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayoonyesha kuwa Rwanda ilitoa msaada wa kijeshi kwa waasi wa M23 Mashariki mwa Congo Novemba mwaka jana.

Akizungumza katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa, Blinken aliahidi kuzungumzia suala hilo wakati wa ziara yake nchini Rwanda.

Alitoa wito kwa pande zote katika eneo hilo kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na serikali ya DRC mashariki mwa Congo. Kundi hilo liliibuka tena mwezi Novemba mwaka jana baada ya takriban muongo mmoja wa kusitisha mapigano.

Serikali ya Rwanda imekana kuwasaidia M23.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani, ambaye yuko katika ziara yake ya pili barani Afrika, aliihakikishia DRC msaada wa Marekani, hasa katika uwekezaji, ili kuhakikisha mbinu bora zaidi zinazingatiwa. Aliisihi Congo kushirikiana na kufanya kazi uwazi wa fedha na haki za kazi kwa sekta ya madini. Marekani iliahidi dola milioni 30 kuisaidia DRC kukuza uwajibikaji na utendaji kazi endelevu wa uchimbaji madini na kuibua wasiwasi kuhusu mnada wa vitalu vya mafuta na gesi vya Congo katika maeneo nyeti.

Mwezi Julai, Reuters iliripoti kwamba haki za kutoa leseni kwa vitalu 30 vya gesi na mafuta nchini DRC zilipigwa mnada, na kufungua sehemu za msitu wa pili kwa ukubwa duniani kwa uchimbaji unaoweza kutoa hewa kubwa ya kabon na kuhatarisha juhudi za kuzuia ongezeko la joto duniani.

Washington na Kinshasa zilikubaliana kuunda vikundi vya kazi juu ya athari za mazingira kwenye minada ya vitalu vya mafuta.

Blinken Jumatano jioni alielekea nchini Rwanda kukamilisha ziara yake katika bara la Afrika.

XS
SM
MD
LG