Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:55

Blinken afanya ziara ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya Syria


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Jumatano ameondoka kwenda Jordan, na baadaye Uturuki kama hatua ya kuyarai mataifa ya kikanda kuwa na msimamo mmoja wa kuisaidia Syria kufuatia kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa kiimla wa muda mrefu Bashar al-Assad.

Kwenye ziara hiyo kwenye miji mikuu ya Aqaba na Ankara, Blinken atakutana na viongozi kutoka mataifa ya Kiarabu, ili kuzungumzia masuala ya Syria, Israel, Gaza na Lebanon na ukanda wa Mashariki ya Kati kwa ujumla, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa Blinken analenga kuwashawishi viongozi wa kanda hiyo kuwa na kauli moja kuhusu mpito wa Syria kufuatia kuondoka kwa Assad. Miongoni mwa kauli hizo ni kuheshimiwa kwa haki za makundi ya walio wachache, upelekaji wa misaada ya kibinadamu, kuizuia Syria kuwa kitovu cha ugaidi au tishio kwa jirani zake, pamoja na kutokomezwa kwa njia salama kwa silaha za kibayolojia au kemikali zilizopo.

Blinken amesema kuwa Marekani itaitambua serikali itakayolinda misingi hiyo. Akizungumza mbele ya kamati ya Bunge ya Masuala ya mambo ya nje Jumatano, Blinken alisema kuwa anaamini kwamba utawala ujao wa rais mteule Donald Trump utahakikisha kulindwa kwa hatua zilizopigwa kuangamiza Khalifa ya kikanda ambayo kundi la Islamic State lilibuni nchini Syria.

Forum

XS
SM
MD
LG