Mazungumzo yao yameangazia namna ya kukabiliana na athari za kuongezeka kwa bei ya chakula Afrika.
Mazungmzo kati ya Blinken na Omamo, yanakuja baada ya mkutano wa New York uliohusu usalama wa chakula duniani ambapo mawaziri walikubaliana kuchukua hatua kupata suluhu la haraka.
Blinken amesisitiza kwamba Marekani itasalia kuwa mshirika mkubwa katika kutafuta suluhu la ukosefu wa chakula duniani.
Mawaziri hao wawili wamezungumzia umuhimu wa Kenya na Marekani kushirikiana katika sekta mbalimbali