Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:41

Blinken aendelea na ziara Beijing


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken yuko Beijing.

Yeye ndiye mwanadiplomasia mkuu wa kwanza wa Marekani kutembelea China tangu 2018.

Blinken anakutana na waziri wa mambo ya nje wa China, Qin Gang, mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi, na kuna uwezekano mkubwa wa kuonana na Rais wa China Xi Jinping.

Maafisa wa Marekani na China wametambua umuhimu wa kuleta utulivu katika uhusiano wa mataifa hayo mwili na kuwa na njia za ngazi ya juu.

Lakini matarajio ni madogo kwa nchi hizo mbili kuweka upya uhusiano unosimama juu ya haki za binadamu, Taiwan, na teknolojia, na masuala mengine ya usalama.

Muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea China, Ijumaa jioni, Blinken aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Washington kwamba maafisa wa Merikani watazungumza waziwazi na wenzao wa China kuhusu wasiwasi walokua nazo kuhusiana na maswala kadhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG