Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:25

Bill Clinton alazwa hospitalini baada ya kuugua mafua


Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton Jumatatu amelazwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Georgetown mjini Washington DC baada ya kuugua mafua.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 alilazwa mida ya adhuhuri ili kufanyiwa vipimo pamoja na uangalizi wa kina. Angel Urena, ambaye ni naibu mkuu wa kiutawala wa Clinton, kupitia taarifa amesema kuwa “Yuu ngali kwenye hali nzuri na kwamba anafurahia huduma za kimatibabu anazopewa Clinton.

Clinton ambaye ni mdemokrat aliyehudumu kwa mihula miwili kama Rais wa Marekani kuanzia Januari 1993 hadi Januari 2001, alihutubia kongamano la kitaifa la chama hicho mjini Chicago msimu wa joto mwaka huu, wakati pia akishiriki kwenye kampeni kuelekea uchaguzi wa Novemba, ambao mgombea wa Demokrat Kamala Harris, alishindwa na mgombea wa Repablikan Donald Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG