Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:11

Biden aanza rasmi shughuli za mpito


US President-elect Joe Biden speaks during a cabinet announcement event in Wilmington, Delaware, on November 24, 2020.
US President-elect Joe Biden speaks during a cabinet announcement event in Wilmington, Delaware, on November 24, 2020.

Shughuli ya mpito ya Rais mteule wa Marekani Joe Biden imeanza rasmi baada ya idara ya serikali kuu - GSA kumtangaza mshindi wa dhahiri wa uchaguzi wa urais wa 2020, wakati Rais Donald Trump akiendelea na jaribio lake la muda mrefu la kutengua ushindi wa Biden kwenye kura.

Timu ya washauri ya Biden mara moja ilianza kuwafikia Jumatatu usiku maafisa wa Trump kote serikalini ili kujua juu ya uwezekano wa vitisho vya usalama wa kitaifa nchi inakabiliwa navyo, na masuala mengine ya haraka ambayo Biden atakabiliwa nayo wakati atakapoapishwa ifikapo Januari 20.

Maafisa wa Pentagon walisema wanachama wa timu ya mpito ya Biden waliwasiliana na Idara ya Ulinzi mara tu baada ya Emily Murphy, msimamizi wa Utawala Mkuu wa Huduma za serikali, kuamua kwamba Biden ndiye mshindi wa dhahiri wa uchaguzi na kwamba mpito unaweza kuanza. Kitendo cha Murphy kinamruhusu sasa Biden kupata fedha za umma kwa kipindi cha mpito, kupokea taarifa za usalama na maafisa wake wa mpito kupata taarifa za idara ya mashirika ya serikali kuu.

Haikufahamika mara moja ni lini Biden atapata fursa ya mkutano wake wa kwanza wa usalama wa kitaifa kama rais mteule. Biden amezungumzia maswala ya usalama na timu yake ya washauri wa ujasusi na wanajeshi lakini bado hajakabidhiwa taarifa ya kila siku ya rais ambayo ni tathmini ya jamii ya ujasusi ya Marekani ya vitisho vya ulimwengu.

Wakati huo huo Gavana wa jimbo la Pennsylvania hapa Tom Wolf alisema Jumanne kuwa Joe Biden amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais katika jimbo hilo. Gavana Wolf aliandika katika ukurasa wake wa tweeter kwamba idara ya mambo ya nje ya Jimbo hilo imethibitisha matokeo ya uchaguzi wa rais na makamu wa rais kama inavyotakiwa na sheria ya serikali kuu, "nimesaini Cheti cha kuthibitisha kwa orodha ya wapiga kura ya Joe Biden na Kamala Harris" aliongeza.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington Dc

XS
SM
MD
LG