Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:59

Biden: Mgogoro kati ya Israel na Palestina lazima upate suluhu


Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas (kulia)
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas (kulia)

Rais wa Marekani Joe Biden ameondoka ukingo wa magharibi akitumia usafiri wa helicopter, na kumaliza sehemu ya kwanza ya ziara yake mashariki ya kati.

Biden ametembelea hospitali ya Palestina mashariki mwa Jerusalem, kukutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas, na kutembelea kanisa mjini Bethlehem ambapo inaaminika kwamba Yesu alizaliwa.

Katika taarifa ya Pamoja akiwa na Abbas, Biden ameahidi kuendelea na juhudi za kupata suluhu la mgogoro wa mda mrefu kati ya Israel na Palestina japo ishara za kupata suluhu hilo zinaonekana kutokuwepo.

"Lazima suluhu ya kisasa ipatikane kwa watu wa Palestina. Hatuwezi kuendelea kuona hali ya fedheha kuendela kuwazingira watu wa Palestina na kuvuruga Maisha yao ya baadaye. Hata kama mazingira ya sasa yanaonekana kutokuwa mazuri kuanza mazungumzo, Marekani na utawala wangu hautakata tamaa katika juhudi zake za kutaka kuwaleta Pamoja Waisrael na wapalestina.” Amesema Biden.

Matamshi yake Biden hata hivyo huenda yasiwafurahishe Wapalestina ambao wanataka Marekani kuilazimisha Isreal kukubali kuanza tena mazungumzo ya amani na Palestina.

Mazungumzo kati ya Israel na Palestina yalivunjika Zaidi ya mwongo mmoja uliopita. Biden amesema kwamba kifo cha mwandishi wa Habari wa Palestina, raia wa Marekani Shireen Abu Akleh, mnamo mwezi May, ilikuwa ni pigo kubwa kutokana na kazi yake ya kuambia uliwengu kuhusu watu wa Palestina.

"Marekani itaendelea kusisitiza kuwepo kwa uajibikaji katika kifo cha mwandishi huyo na tutaendelea kutetea uhuru wa vyombo vya Habari kila mahali duniani.”

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema mapema mwezi huu kwamba huenda Abu Akleh aliuawa kwa risasi iliyofyatuliwa kutoka Israel , alipokuwa anaripoti kuhusu oparesheni ya kijeshi kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, ukanda wa magharibi.

Biden anafanya mkutano na viongozi wa Saudi Arabia katika sehemu ya pili ya ziara yake mashariki ya kati, ambapo wanazungumzia kuhusu usafirishaji wa mafuta, haki za kibinadamu, na ushirikiano wa kiusalama.

XS
SM
MD
LG