Afisa wa ngazi ya juu kwenye utawala wa Biden amewaambia wanahabari kwamba pande zote mbili zinatarajiwa kutangaza juhudi za pamoja za kuimarisha miundombinu ya mpakani ili kuzuia uhamiaji haramu pamoja na upitishaji wa dawa za kulevya, na kuhakikisha nishati safi, ukuaji wa uchumi pamoja na ustawi.
Ripoti zimeongeza kwamba watazindua jopokazi la kutadhmini mikakati ya uhamiaji pamoja na ulinzi wa wafanyakazi. Mkuu wa baraza la usalama la taifa, kwa ajili ya ukanda wa magharibi Juan Gonzalez ameiambia VOA Jumatatu kwamba ikulu ya Marekani inatadhmini kuongeza idadi ya vibali kwa wafanyakazi wa muda kutoka Mexico na mataifa mengine ya amerika ya kati.