Uekezaji huo umetangazwa wakati wa mkutano wa viongozi wa UAE, India na Marekani, uliofanyika kwa njia ya video.
Akizungumza akiwa Jerusalem, rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba ufadhili huo unaweza kuongoza mazao ya chakula katika eneo hilo, mara tatu ya ilivyo sasa katika mda wa miaka 5.
"Miradi miwili ya kwanza kuhusu chakula na nshati safi ambayo tunashirikiana, ina lengo la kumaliza mgogoro ya dharura ambayo watu wanakumbana nayo kwa sasa kote duniani. Uekezaji unaofanywa na umoja wa falme za kiarabu katika maeneo ya kukuza chakula kote India kwa ushirikiano na sekta ya kibianfsi ya Marekani na Israel, una uwezo wa kuimarisha uzalishaji wa chakula mara tatu Zaidi ya ilivyo sasa katika mda wa miaka mitano.” Amesema Biden
Nchi hizo nne zitawekeza pia katika miradi ya nshati nchini India.
Biden amesema kwamba amesema kwamba miradi hiyo itashirikisha sekta binafsio za India na Marekani.
Kongamano hilo limefanyika wakati dunia inakabiliwa na ukosefu wa chakula kutokana na vita vinavyoendelea Ukraine.
Kabla ya kongamano hilo, Biden amekutana na waziri mkuu wa Israel Yair Lapid, na kusaini mkataba wa kiusalama dhidi ya Iran, kabla ya viongozi hao wawili kuhutubia waandishi wa Habari mjini Jerusalem.
"Leo tumezungumzia kujitolea kwa Marekani kuhakikisha kwamba Iran haitawahi kuwa na silaha za nuclear. Haya ni maslahi muhimu sana ya kiusalama kwa Israel, Marekani, na kwa dunia nzima. Nitaendelea kuamini kwamba diplomasia ndio njia nzuri kabisa ya kupata mwafaka.”
Rais Biden anatarajiwa Saudi Arabia kesho ijumaa, baada ya kufanya mazungumzo na rais wa Palestina Mahmud Abbas katika ukingo wa magharibi.