Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 04:08

Biden atoa msamaha kwa bata mzinga wawili wakati wa Siku Kuu ya Shukrani


Bata mzinga Blossom na Peach waliosamehewa na Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu.
Bata mzinga Blossom na Peach waliosamehewa na Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu alianza mkondo wa mwisho wa msimu wa sherehe akiwa madarakani kweye White House kwa kutoa msamaha kwa bata mzinga wawili ambao hawatachinjwa wakati wa Sikukuu ya Kutoa Shukurani mwishoni mwa wiki, wakiwa kusini mwa jimbo la Minnesota.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu alianza mkondo wa mwisho wa msimu wa sherehe akiwa madarakani kweye White House kwa kutoa msamaha kwa bata mzinga wawili ambao hawatachinjwa wakati wa Sikukuu ya Kutoa Shukurani mwishoni mwa wiki, wakiwa kusini mwa jimbo la Minnesota. Biden alikaribisha wageni 2,500 kwenye bustani ya South Lawn kwenye Ikulu, wakati akitania kuhusu bata hao kwa jina Peach na Blossom, wakati pia akizungumzia wiki zake za mwisho za utawala baada ya kuwa kwenye uongozi mjini Washington kwa nusu karne.

Biden alisema kuwa daima atakuwa mwenye shukrani hadi atakapoondoka Januari 20 ili kumpisha rais mteule Donald Trump. Hadi wakati huo, Biden na mke wake Jill Biden wataendelea na shughuli za msimu wa siku kuu wakati pia wakijiandaa kuondoka kwenye Ikulu. Mke wa Biden Jill Biden Jumatatu alipokea rasmi mti wa Krismasi wa Ikulu ya Marekani ambao utarembeshwa na kuwekwa kwenye chumba cha Blue. Mti huo wenye urefu wa mita 5.64 kwa jina Fraser ulitoka kwenye shamba moja magharibi mwa jimbo la North Carolina, ambako kimbunga Helene kiligonga hivi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG