Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 10:01

Biden atembelea Florida Jumapili kujionea hasara ya kimbunga Milton


Biden akitoa hotuba yake baada ya kutembelea waathiriwa wa Milton jimboni Florida Jumapili.
Biden akitoa hotuba yake baada ya kutembelea waathiriwa wa Milton jimboni Florida Jumapili.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili alijionea mwenyewe hasara iliosababishwa na kimbunga Milton, kwenye jimbo la Florida, ambapo baadhi ya wakazi wanaendelea kutafakari uharibifu wa kimbuga Helen kilichotokewa mwishoni mwa Septemba.

“Eneo hilo limeathiriwa vibaya na vimbunga vilivyofuatana,” Biden alisema baada ya kujionea hali akiwa kwenye helikopta ya Marine One, katika ufukwe wa magharibi mwa Florida kuanzia Tampa hadi St Petersburg.

Jumla ya watu 17 wamekufa jimboni humo kutokana na kimbunga hicho, wengi wao ikiwa ni kutokana na upepo mkali uliosababishwa na kimbunga hicho. Akiwa ardhini Biden alijionea vifusi vilivojaa barabarani pamoja na miti ilioanguka. Kiongozi huyo pia alipongeza wakazi wa magharibi mwa Florida kwa kusaidiana wakati wa janga hilo. Alisema pia kuwa umeme umerejeshwa kwa wakazi milioni mbili kati ya takriban milioni 3 walioathiriwa na kimbunga Milton.

Alisema kuwa maelfu ya wafanyakazi wa umeme kutoka majimbo 43 pamoja na Canada wapo kwenye jimbo hilo ili kukarabati mifumo ya umeme. Masaada wa dola milioni 612 kutoka kwa serikali kuu ulitangazwa kwa ajili ya kusaidia waathirika wa vimbunga Helene na Milton. Idara ya kitaifa ya Hali ya Hewa imesema kuwa mafuriko yanatarajiwa kuendelea kwenye maeneo ya Tampa Bay na Sanford kutokana na kuongezeka kwa maji ya mito.

Forum

XS
SM
MD
LG