Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:58

Biden atangaza mpango wa kupunguza uzalishaji wa gesi ya Methane


Rais wa Marekani, Joe Biden katika mkutano wa hali ya hewa (COP26) huko Glasgow, Nov. 2, 2021.
Rais wa Marekani, Joe Biden katika mkutano wa hali ya hewa (COP26) huko Glasgow, Nov. 2, 2021.

Methane mojawapo ya gesi za Hydrocarbon ni gesi inayochangia katika ongezeko la joto duniani na huzalishwa katika usafirishaji na uzalishaji wa makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta. Mifugo, maeneo ya kutupa taka na tabia za kilimo pia huzalisha kiasi kikubwa cha gesi

Rais wa Marekani Joe Biden, leo Jumanne alitangaza mpango mpana wa Marekani wa kupunguza uzalishaji wa gesi ya Methane huku viongozi kutoka zaidi ya mataifa 100 wakikutana kwa siku ya pili ya mazungumzo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Glasgow.

Methane mojawapo ya gesi za Hydrocarbon ni gesi inayochangia katika ongezeko la joto duniani na huzalishwa katika usafirishaji na uzalishaji wa makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta. Mifugo, maeneo ya kutupa taka na tabia za kilimo pia huzalisha kiasi kikubwa cha gesi.

Leo Jumanne utawala ulizindua mpango unaounganisha sekta tofauti za serikali ya Marekani ikiwa ni pamoja na idara ya nishati, kilimo, uchukuzi, nyumba na mambo ya ndani kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Mpango huu unapaswa kuileta Marekani kua pamoja na ahadi ya dunia kupunguza Methane ambapo wazalishaji wakubwa zaidi duniani wanalenga kupunguza uzalishaji wa jumla wa Methane kwa asilimia 30 chini ya viwango vya mwaka 2020 ifikapo mwaka 2030.

XS
SM
MD
LG