Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 12, 2024 Local time: 10:51

Biden asifu hatua zilizopigwa kuelekea afya ya wanawake Marekani


Rais wa Marekni Joe Biden akizungmza wakati wa kongamano la utafiti wa afya ya wanawake kwenye ikulu White House mjini Washington, Dec. 11, 2024.
Rais wa Marekni Joe Biden akizungmza wakati wa kongamano la utafiti wa afya ya wanawake kwenye ikulu White House mjini Washington, Dec. 11, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amesema kuwa anajivunia kuona kwamba program ya utafiti wa afya ya wanawake aliyoianzisha  mwaka jana kupitia ushawishi wa mke wake, tayari imewekeza karibu dola bilioni moja, kwa kuwa afya njema kwa wanawake inaimarisha ustawi wa Marekani.

“Huo ndiyo ukweli,” alisema kwenye hotuba yake ya mwisho ya kufunga kongamano la kwanza na White House kuhusu Utafiti wa Afya ya Wanawake. Hata hivyo alisema kuwa bado hatujafikisha jitihada hizo kwa timu nyingine, akiwa na maana ya utawala ujao wa rais mteule Donald Trump. Wateuliwa watatu wa Trump kwenye Mahakama ya Juu wakati wa muhula wake wa kwanza walipiga kura ya kuondoa haki ya kikatiba ya wanawake kutoa mimba.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, wademokrat walifanya kampeni zao kupitia wito wa haki za afya ya uzazi na ya wanawake. Msemaji wa timu ya mpito ya Trump Karoline Leavitt, alisema kwamba rais mteule ataweka ahadi yake ya kuimarisha mfumo wa afya wa Marekani. “Trump alifanya kampeni kwa kuahidi kuimarisha afya wa Wamarekani wote wakiwemo wanaume, wanawake na watoto, na atatimiza ahadi hiyo,” Leavitt alisema kupitia ujumbe wa barua pepe.

Forum

XS
SM
MD
LG