Kiongozi huyo alifanyiwa vipimo Jumamosi baada ya kupona kutokana na maambukizi ya wiki iliyopita, akisemekana kuendelea kujiweka kwenye karantini katika ikulu ya White House baada, ya maambukizi hayo mapya kugundulika, Dkt Kevin O Connor ameongeza kwenye taarifa.
O Connor amesema kwamba Biden mwenye umri wa miaka 79 ana dhamira ya kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa karibu naye wanalindwa dhidi ya maambukizi. Daktari huyo amesema kwamba Biden alikuwa amepona kutokana na maambukizi ya awali ,lakini yakarudi tena, suala analosema hujitokeza kwa asilimia ndogo ya wagonjwa wanaotumia dawa aina ya Paxlovid kutibu maambukizi ya awali.
Mshauri mkuu wa kifya wa Rais amesema kwamba hali ya kupatikana kuwa na virusi baada ya kupata chanjo haina historia ya kuwa na hatari yoyote. Biden ataendelea kufanyia kazi kwenye ofisi yake wakati leo akilazimika kuahirisha ziara iliyokuwa impeleke kwenye jimbo lake la Delaware.