Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:17

Biden anamkaribisha mfalme Abdullah wa Jordan huko White House


Biden APEC Informal Summit on COVID Vaccine Sharing 2
Biden APEC Informal Summit on COVID Vaccine Sharing 2

Itakuwa ni fursa kujadili changamoto nyingi zinazoikabili mashariki ya kati na kuonyesha jukumu la uongozi wa Jordan katika kuhamasisha amani na uthabiti katika eneo msemaji wa White House, Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari. Aliita Jordan ni mshirika muhimu wa usalama na mshirika wa Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden anamkaribisha mfalme Abdullah wa Jordan huko White House leo Jumatatu huku masuala kadhaa muhimu ya kieneo yakiwa kwenye ajenda pamoja na kuonyesha uungaji mkono kwa kiongozi huyo wa Jordan baada ya changamoto kwa utawala wake.

Itakuwa ni fursa kujadili changamoto nyingi zinazoikabili mashariki ya kati na kuonyesha jukumu la uongozi wa Jordan katika kuhamasisha amani na uthabiti katika eneo msemaji wa White House, Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari. Aliita Jordan ni mshirika muhimu wa usalama na mshirika wa Marekani.

Mfalme Abdullah wa Jordan
Mfalme Abdullah wa Jordan

Mikutano ya Jumatatu inatarajiwa kujumuisha majadiliano ya hali nchini Syria mahala ambako mzozo wa muongo mmoja umewasukuma zaidi ya wa-Syria milioni moja kuingia Jordan pamoja na nchi Jirani ya Iraq ambako majeshi ya Marekani yamekuwa yakilengwa na mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

XS
SM
MD
LG