Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 04:51

Biden afuta hukumu ya kifo kwa wafungwa 37


Rais wa Marekani, Joe Biden.
Rais wa Marekani, Joe Biden.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu ameondoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 37 kati ya 40 waliyokuwa wamehukumiwa na mahakama ya serikali kuu, hatua inayodhihirisha upinzani  wake kwa hukumu hiyo kwa muda mrefu.

Hatua hiyo pia inanyima utawala ujao wa Trump nafasi ya kuamuru kunyongwa kwa wafungwa hao. Utawala wa kwanza wa Trump aliamuru kunyongwa wa wafungwa 13 waliyopewa hukumu ya kifo, ikiwa idadi kubwa zaidi ndani ya muhula mmoja wa rais. Watu hao 37 waliyoondoleawa hukumu ya kifo sasa watabaki jela maisha yao yote, bila kuwa na matumaini ya msamaha wa kufunguliwa, kwa kuwa mahakama iliwapata na hatia za kuangamiza maisha ya wengine.

Wengi miongoni mwao wamesubiri kunyongwa kwa zaidi ya muongo mmoja. “Msinielewe vibaya, nakemema mauaji yaliotendwa nao, pamoja na uchungu waliyosababishia familia za waathirika, “ alisema Biden, akiongeza kuwa, “ nikiongozwa na nafsi yangu ya kulinda haki za umma, kama mwenye kiti wa kamati ya Sheria ya Seneti, makamu wa rais na sasa rais, nimeshawishika kwamba tunahitaji kumaliza hukumu ya kunyonga kwenye ngazi za serikali kuu.” Sitokubali kuona utawala mpya ukirejea kunyonga watu, hatua mbayo nilisitisha, ameongeza kusema.

Forum

XS
SM
MD
LG