Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:27

Biden aendelea kuweka historia katika uteuzi wake


Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameteua maafisa wa ngazi ya juu kusimamia uchumi wa Marekani unaoathiriwa na janga la virusi vya Corona.

Miongoni mwa walioteuliwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani Janet Yellen, ambaye anakuwa mwanake wa kwanza kuwa waziri wa fedha katika historia ya miaka 231 ya wizara hiyo.

Biden amemteua Neera Tanden, kuwa mkuu wa ofisi ya kusimamia utawala na bajeti ya serikali. Iwapo ataidhinishwa na senate, Tanden atakuwa mwanamke wa kwanza, Mmarekani mwenye asili ya Afrika kuongoza Idara hiyo.

Wally Adeyemo, ameteuliwa kuwa naibu wa waziri wa fedha, akiwa mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuteuuliwa katika nafasi hiyo.

Wengine walioteuliwa ni Pamoja na mchumi Cecilia Rouse, kuwa mkuu wa baraza la washauri wa uchumi katika white house.

Anakuwa mwanamke wa kwanza, mmarekani mwenye asili ya Afrika kushikilia nafasi hiyo.

Janga la Corona limeathiri sana uchumi wa Marekani ambao ndio mkubwa zaidi duniani.

Wanawake wameteuliwa kuongoza timu nzima ya mawasiliano white house.

Ushindi wa Biden waidhinishwa Arizona

wakati huo huo viongozi wa jimbo la Arizona wameidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden na kuendeleza ushindi wa Biden katika majimbo ambayo rais Donald Trump amekuwa akidai kwamba kulifanyika wizi wa kura bila kutoa Ushahidi wowote.

Biden ameshinda kura 11 za wajumbe katika jimbo hilo, baada ya kupata zaidi ya kura 10,000 ya alizopata Trump.

Biden anakuwa mgombea wa kwanza wa urais wa chama cha democratic kushinda jimbo hilo tangu mwaka 1996.

Waziri wa mambo ya nje wa jimbo la Arizona Katie Hobbs, ameidhinisha matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo.

Hobbs, ambaye ni mdemocrat, ametangaza matokeo hayo akiwa Pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa chama cha Republican.

Viongozi hao wamesema kwamba uchaguzi mkuu katika jimbo hilo ulikuwa wa kweli, sahihi na ulifuata sheria za uchaguzi za jimbo la Arizona.

Biden anatarajiwa kuapishwa Januari tarehe 20 na kuwa rais wa 46 wa Marekani.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG