Ukulu ya Marekani imesema kuwa wanajeshi hao watasaidia katika kupeleka chakula , maji pamoja na bidhaa nyingine muhimu kwa waathirika. Upelekaji huo pia utaongeza idadi ya maafisa wa uokozi pamoja na kusaidia idara ya kitaifa ya dharura , FEMA na mashirika mengine kufikia watu waliopo kwenye maeneo yalioathiriwa zaidi.
Rais Joe Biden na makamu wake Kamala Harris Jumatano wametembelea maeneo yalioathiriwa, rais akianza na majimbo ya North na South Carolina ambapo alizungumza na waokozi pamoja na maafisa wa majimbo hayo. Harris naye alitembelea Georgia wakati akikutana na maafisa pamoja na wakazi wa jimbo hilo.
Majimbo ya North na South Carolina yamebaki bila huduma muhimu kama umeme na mawasiliano ya simu, huku timu za waokozi zikiendelea kutafuta watu waliotoweka kufuatia kimbunga hicho ambacho tayari kimeua takriban watu 166. Zaidi ya wakazi milioni 1.2 kufikia Jumatano hawakuwa na umeme kwenye majimbo yalioathiwa.
Forum