Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 04:08

Benki ya Dunia yasitisha ufadhili wa mradi wa utalii na uhifadhi nchini Tanzania


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokutana na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris huko White House Aprili 15, 2022, mjini Washington.AP.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokutana na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris huko White House Aprili 15, 2022, mjini Washington.AP.

Benki ya Dunia ilisema Jumanne kuwa imesitisha ufadhili wa mradi wa utalii na uhifadhi nchini Tanzania kufuatia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mradi wa Natural Resilient for Tourism and Growth Project (REGROW) wenye thamani ya dola milioni 150 ulianzishwa kwa lengo la kuboresha usimamizi wa maliasili na mali za utalii kusini mwa Tanzania, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Lakini Taasisi ya Oakland, taasisi yenye makao yake makuu nchini Marekani, iliibua madai mwaka jana ya kufukuzwa kwa nguvu na ukiukwaji wa haki dhidi ya jamii zinazoishi karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo serikali inapanga kupanua kama sehemu ya mpango huo.

Benki ya Dunia ilisema ina wasiwasi mkubwa kuhusu madai ya unyanyasaji na ukosefu wa haki kuhusiana na mradi wa REGROW.

Serikali ya Tanzania bado haijatoa maoni hadharani.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inasifika kwa mbuga zake za kuvutia za wanyama kama Serengeti, na pia kuwa eneo ulipo kwa mlima mrefu zaidi barani Afrika, Kilimanjaro na visiwa vya Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na Zanzibar.

Sekta ya utalii ilizalisha mapato ya dola bilioni 3.37 mwaka 2023 huku wageni waliopokeklewa kimataifa wakiongezeka kwa asilimia 24 hadi milioni 1.8, kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Forum

XS
SM
MD
LG