Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:58

Benki ya Dunia : Uchumi wa Afrika umeshuka hadi asilimia 2.7


Ramani ya Afrika
Ramani ya Afrika

Benki ya Dunia imepunguza matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa eneo la Afrika chini ya jangwa la Sahara mwaka 2018 hadi asilimia 2.7 badala ya utabiri wa awali wa asilimia 3.1, kwa kiasi kikubwa kutokana na ukuaji wa pole pole kwa uchumi katika bara hilo, taarifa ya benki imesema Jumatano.

Eneo hilo, ambalo lilikuwa na ukuaji wa viwango vya wastani vya uchumi miaka kadhaa kuelekea mwaka 2015, ilipata hasara kubwa katika kasi ya ukuaji wake baada ya bei za bidhaa kushuka mwaka 2015 – 2016.

Mwezi Aprili, Benki ya Dunia ilibashiri kwamba ukuaji huenda ungekuwa kwa kasi zaidi mwaka 2018, ukuaji wa wastani ukiwa katika kiwango cha asilimia 3.1, ikiwa ni juu kutoka ukuaji wa asilimia 2.3 mwaka 2017.

“Kasi ya ukuaji wa pole pole barani Afrika chini ya jangwa la Sahara unaelezewa unatokana na upanuzi usiotabirika wa kiuchumi katika mataifa matatu yenye uchumi mzuri ya Nigeria, Angola na Afrika Kusini,” taarifa ya benki imesema.

Kushuka kwa uzalishaji mafuta nchini Angola na Nigeria kumepelekea kupanda kwa bei za mafuta, na nchini Afrika Kusini, ukuaji dhaifu wa matumizi ya majumbani kumetokana na kupungua kwa shughuli za kilimo, taarifa ya Benki ya Dunia imesema.

Nchi nyingine katika bara hilo zimekuwa na ukuaji usiotetereka mwaka 2018, benki imesema, ikiwemo zile ambazo hazitegemei bidhaa, kama vile Ivory Coast, Kenya na Rwanda.

Albert Zeufack, mchumi mkuu kwa Afrika katika Benki ya Dunia, amezisihi serikali katika eneo hilo kuachakutumia fedha vibaya na badala yake kuboresha uzalishaji ili kusaidia katika harakati za kufufua uchumi.

Madeni makubwa ya umma katika baadhi ya nchi kwenye bara hilo, ukichanganya na sarafu dhaifu na kupanda kwa viwango vya riba, huenda kukahatarisha uwezo wa kulipa madeni yao, Benki ya Dunia imeonya.

“Watunga sera katika eneo hilo lazima wajiweke sawa kukabiliana na hatari mpya ambazo zinajitokeza kutokana na mabadiliko katika mtiririko wa mitaji na madeni,” Zuefack amesema.

XS
SM
MD
LG