Benki ilipandisha kiwango cha sera yake kwa asilimia 5, hadi 40 na hivyo kuashiria ongezeko lake la sita la riba mfululizo likilenga kupunguza mfumuko wa bei ambao ulifikia asilimia 61.36 mwezi uliopita.
Hata hivyo, benki hiyo ilisema nyongeza yake ya viwango itaisha hivi karibuni. Benki kuu imeeleza kiwango cha sasa cha kubana fedha kiko karibu sana na kiwango kinachohitajika ili kuanzisha mzunguko wa kupunguzwa kwa bei benki hiyo imesema.
Rais Recep Tayyip Erdogan kwa muda mrefu amekuwa mtetezi wa sera ya kupunguza viwango vya riba ili kupambana na mfumuko wa bei na aliwafuta kazi magavana wa benki kuu ambao walipinga sera zake za kupunguza viwango vya riba.
Forum