Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:24

Benki kuu ya Nigeria yaongeza muda wa mwisho wa kubadilisha noti za zamani za naira


Mtu akiwa ameshika noti mpya ya Naira 1000 huku Benki Kuu ya Nigeria ikitoa noti hizo kwa umma kupitia benki za Abuja.Desemba 15, 2022. REUTERS
Mtu akiwa ameshika noti mpya ya Naira 1000 huku Benki Kuu ya Nigeria ikitoa noti hizo kwa umma kupitia benki za Abuja.Desemba 15, 2022. REUTERS

Benki kuu ya Nigeria itaongeza kwa siku 10 zaidi muda wa mwisho wa kubadilisha noti za zamani za naira, ilisema katika taarifa yake Jumapili.

Raia wa Nigeria sasa watakuwa na hadi Februari 10 kurejesha noti za naira 1,000, 500 na 200. Benki kuu (CBN) ilianza kutoa noti mpya iliyotengenezwa mwezi uliopita lakini wengi wanasema hawawezi kuzipata kwenye benki au mashine za kutolea fedha.

Gavana wa Benki kuu nchini humo - CBN Godwin Emefiele, katika taarifa yake, alisema tarehe ya mwisho mpya itawaruhusu zaidi wale walio katika jamii za vijijini kubadilishana noti za zamani.

Baada ya tarehe ya mwisho ya Februari 10, taarifa hiyo ilisema, Wanigeria watakuwa na siku saba zaidi za kuweka noti za zamani moja kwa moja kwa CBN.

Wabunge wa Nigeria na mgombea urais wa upinzani Atiku Abubakar wameitaka Benki Kuu kuongeza muda wa Januari 31. Mgombea huyo alisema kwamba kuongezwa kwa muda kutasaidia katika kupunguza athari za kifedha kwa raia.

XS
SM
MD
LG