Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 02:22

Benki kuu Libya imesitisha shughuli hadi afisa aliyetekwa nyara atakapoachiliwa


Ramani ya Libya na miji yake
Ramani ya Libya na miji yake

Benki Kuu ni taasisi pekee inayotambuliwa kimataifa kwa mapato ya mafuta ya Libya, mapato muhimu ya uchumi wa nchi hiyo

Benki kuu ya Libya yenye makao yake mjini Tripoli imesema leo Jumapili itafunga shughuli zote na haitaanza kazi hadi afisa mwandamizi wa benki hiyo aliyetekwa nyara mapema leo atakapoachiliwa.

Benki Kuu ni taasisi pekee inayotambuliwa kimataifa kwa mapato ya mafuta ya Libya, mapato muhimu ya uchumi kwa nchi hiyo iliyogawanyika kwa miaka mingi kati ya serikali mbili hasiju huko mjini Tripoli na Benghazi. Benki hiyo imesema kundi lisilojulikana lilihusika na utekaji nyara leo Jumapili wa Musaab Muslam, mkuu wa idara ya teknolojia ya habari.

“Benki hiyo inapinga mbinu kama vile za kibabe ambazo zinafanywa na baadhi ya makundi nje ya sheria,” ilisema taarifa hiyo. iliongeza kuwa maafisa wengine wa benki hiyo pia wametishiwa na hivyo watasimamisha shughuli hadi zoezi hili litaktabia hizi zitakaposita na mamlaka zinazohusika kuingilia kati.

Forum

XS
SM
MD
LG