Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:44

Benin: Upinzani waruhusiwa kushiriki uchaguzi wa bunge kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne


Rais wa Benin Patrice Talon na makamu rais Mariam Chabi Talata wakishiriki hafla ya kuapishwa, Mei 23, 2021. Picha ya AFP
Rais wa Benin Patrice Talon na makamu rais Mariam Chabi Talata wakishiriki hafla ya kuapishwa, Mei 23, 2021. Picha ya AFP

Benin Jumapili ilifanya uchaguzi wa bunge jipya huku wagombea wa upinzani wakiruhusiwa kugombea kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne chini ya utawala wa Rais Patrice Talon, ingawa idadi ya waliojitokeza haikutangazwa.

Uchaguzi wa Jumapili ulikuwa mtihani mkubwa kwa taifa hilo la Afrika Magharibi, ambapo wafuasi wa Talon wanasema alileta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi, huku wakosoaji wakieleza kuwa muhula wake ulidhoofisha demokrasia.

Kulikuwa na hali ya utulivu kwenye barabara za mji mkuu wa kiuchumi, Cotonou, masoko na maduka yote yalikuwa yamefungwa, waandishi wa AFP walisema.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa kumi alasiri kwasaa za huko, lakini muungano wa mashirika ya kiraia ulisema vituo vingi vilifunga kwa kuchelewa.

Uchaguzi wa mwisho wa bunge wa mwaka 2019 uligubikwa na machafuko mabaya, idadi kubwa ya watu ambao hawakupiga kura na kufungwa kwa mtandao wa intaneti, matukio nadra nchini Benin, ambayo awali ilipongezwa kuwa kitovu cha demokrasia eneo la Afrika magharibi.

Upinzani haukuweza kushiriki kwenye uchaguzi wa 2019.

XS
SM
MD
LG