Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:17

Belarus kutuma wanajeshi wake kushirikiana na Russia kupambana na Ukraine


Rais wa Russia Vladmir Putin (kushoto) na mwenzake wa Belarus Alexander Lukashenko baada ya mkutano wao St. Petersburg June 25 2022.
Rais wa Russia Vladmir Putin (kushoto) na mwenzake wa Belarus Alexander Lukashenko baada ya mkutano wao St. Petersburg June 25 2022.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ametangaza kwamba amewaamuru wanajeshi wake kuungana na wanajeshi wa Russia kwenye mpaka wake na Ukraine, ili kujibu kile amekitaja kama ni tishio la wazi kutoka kwa Ukraine na nchi za magharibi kutaka kuivamia.

Matamshi ya Lukashenko ambaye ametawala Belarus tangu mwaka 1994, yanaashiria kueneza vita vinavyoendelea Ukraine, huku kukiwepo dalili ya wanajeshi wa Russia kuungana na Belarus katika kushambulia sehemu za kaskazini mwa Ukraine.

"Mazungumzo kuhusu namna ya kuishambulia Belarus yanafanyika na kupangwa nchini Ukraine,” amesema Lukashenko bila kutoa ushahidi wowote, katika kikao cha usalama. "Washirika wao wanawasukuma kuanza vita dhidi ya Belarus na kutulazimu kuanza kupigana.”

"Tumekuwa tukijitayarisha kwa hilo kwa miongo kadhaa. Ikihitajika, tutajibu,” ameendelea kusema Lukashenko, na kusema kwamba amezungumza na rais wa Russia Vladimir Putin kuhusu hali hiyo.

Jeshi la kiukanda kati ya Belarus na Russia

Majoezi ya wanajeshi wa Russia na Belarus Februari 17 2022
Majoezi ya wanajeshi wa Russia na Belarus Februari 17 2022

Lukashenko amesema kwamba amekubaliana na Putin kutuma jeshi la kiukanda na kwamba jeshi hilo limeanza ushirikiano siku mbili zilizopita.

Ushirikiano wa kijeshi kati ya Belarus na Russia unajiri siku mbili baada ya daraja la linalounganisha Russia na Crimea, mapema jumamosi.

Lukashenko amesema kwamba Belarus ilipata onyo kutoka kwa vyanzo visivyo rasmi kwamba Ukraine ilikuwa inapanga kutekeleza shambulizi jingine dhidi ya barabara (daraja).

Hajatoa maelezo zaidi.

"Jibu langu lilikuwa rahisi: mwambie rais wa Ukraine na wendawazimu wengine kwamba wakijaribu kuguza hata mita moja ya sehemu ya ardhi yetu, watajuta.” Amesema Lukashenko.

Ukubwa wa jeshi la Belarus

Wanajeshi wa Belarus wakipokea mafunzo katika kambi ya Belarus March 8 2022
Wanajeshi wa Belarus wakipokea mafunzo katika kambi ya Belarus March 8 2022

Jeshi lina Belarus lina wanajeshi 60,000.

Mapema mwaka huu, Belarus ilituma vikosi sita vya wanajeshi wa kimkakati, ambao ni maelfu ya wanajeshi, kwenye mipaka yake.

Mkuu wa jeshi la Belarus anayesimamia usimamizi wa mipaka ameishutumu Ukraine kwa kile amekitaja kama uchokozi.

Wanajeshi wa Russia wanatumia sehemu ya Belarus kupanga na kutekeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine tangu Februari 24.

Sehemu hiyo uinatumika kutuma vifaa vya kijeshi na wanajeshi kaskazini mwa Ukraine.

XS
SM
MD
LG