Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:52

Belarus inatoa msaada wa kijeshi wa Russia kushambulia Ukraine


Mazoezi ya kijeshi kati ya Belarus na Russia Feb 19,2022
Mazoezi ya kijeshi kati ya Belarus na Russia Feb 19,2022

Wafuatiliaji wa shughuli za kijeshi wamesema kwamba rais wa Belarus Alexander Lukashenko anatoa msaada wa kijeshi na silaha kwa Russia katika vita vinavyoendelea Ukraine.

Belarus imeruhusu karibu wanajeshi wa Russia waliosajiliwa hivi karibuni kupokea mafunzo nchini humo, huku ikitoa karibu silaha nzito 211 kwa Russia.

Kiongozi wa upinzani Sviatlana Tsikhanouskaya ameambia VOA kwamba rais Lukashenko anaendelea kutoa msaada kwa Rafiki wake mkubwa, rais wa Russia Vladimir Putin.

Tshikhanouskaya amesema kwamba Lukashenko anatumia msaada huo kama mkakati wa kisiasa kuendelea kukaa madarakani na kutaka kuonyesha kwamba ni mwaminifu kwa Putin.

Russia imekuwa ikitumia Belarus kupanga mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Wafuatiliaji wa shughuli za kijeshi nchini Belarus, ikiwemo Hajun, wamesema kwamba idadi ya wanajeshi wa Russia nchini Belarus inaendelea kuongezeka na kuna ripoti kwamba kambi za kijeshi za Belarus zina idadi kubwa ya wanajeshi kuzidi kiasi na kwamba Russia imeanza kujenga kambi mpya ili kuendelea kutuma nchini humo wanajeshi zaidi.

XS
SM
MD
LG