Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema walinda amani wa kimataifa wamesaidia serikali ya Somalia kupata mafanikio makubwa ya usalama huko Mogadishu lakini amesema wanahitaji kuongeza wanajeshi zaidi ili kudumisha usalama katika maeneo mengine ya nchi.
Bw. Ban alitoa maelezo hayo jana baada ya ziara fupi huko Somalia , ikiwa ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa Umoja wa Mataifa katika zaidi ya miaka 18. Alisema ziara hiyo yake ni ishara ya kuimarisha kwa hali ya usalama.