Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:43

BAL: REG ya Rwanda watoka kifua mbele dhidi ya Kwara Falcons ya Nigeria


Mabingwa wa kikapu Nigeria Kwara Falcons, wapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa wa Rwanda REG.
Mabingwa wa kikapu Nigeria Kwara Falcons, wapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa wa Rwanda REG.

Wawakilishi wa Rwanda katika michuano ya BAL Rwanda Energy Group (REG) wameibuka na ushindi dhidi ya mabingwa wa Nigeria Kwara Falcons kwa jumla ya pointi 64-48 siku ya Jumapili katika uwanja wa Dakar Arena Senegal.

Timu ya Falcons ilipambana kujaribu kurudi mchezoni ikiwa pointi 12 nyuma katika kota ya pili na kufanikiwa kufikisha pointi 31-31 mapema katika kota ya tatu.

Hata hivyo, kurudi huko kuliwaamsha REG, ambao walijibu kwa kupachika pointi 15 bila majibu na kupata ushindi katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi ya Kikapu Afrika kanda ya Sahara.

“Mchezo mmoja haututambulishi sisi ni nani alisema Wilson Jr. kwa kujiamini na kuongeza “tunapaswa kurekebisha kile tunachohitaji kurekebisha na kuja kwa mashambulizi makali katika mchezo wetu unaofuata.”

Kwa mara ya pili katika historia ya BAL, timu ya Nigeria ilipoteza mchezo wao wa ufunguzi katika mashindano hayo.

Miaka miwili iliyopita, timu ya Rivers Hoopers ya Nigeria ilifungwa na Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Patriots ya Rwanda kwenye mechi ya ufunguzi wa BAL mjini Kigali.

Matumaini na ari ya kupambana vitakuwa muhimu kwa Kwara Falcons ikiwa wanataka kufikia mechi za mtoano za BAL, jambo ambalo Hoopers walishindwa kutimiza.

“Lolote linaweza kutokea. Tayari tumethibitisha kuwa sisi tunastahili kuwa hapa," Wilson Jr, aliendelea kusema.

Adonis Filer, Cleveland Thomas Jr na Delwan Graham waliendeleza mashambulizi ya REG, wakifunga kwa pamoja pointi 40 kati ya 64 za mabingwa hao wa Rwanda.

Mchezaji wa kimataifa wa DRC Pitchou Manga alionyesha ukali wake kwenye eneo la ufungaji akimalizia kwa kupata ribaundi 12, Kuzuia mara 4 na kuweka nyavuni pointi 7 kwa timu ya REG.

“Mimi si mgeni kwenye BAL. Kwa hivyo najua nini cha kutarajia, na nilifanya niwezavyo ili kusaidia timu yetu kushinda mchezo wetu wa kwanza wa msimu wa BAL. Ilikuwa nzuri sana kuanza na ushindi” Manga aliongeza.

Wakati huo huo, Jawad Adekoya mchezaji pekee wa Falcons pekee wa Kwara Falcons kufunga pointi za tarakimu mbili alimaliza na pointi 15.

Mchezaji wa REG Adonis Filer alikubali juhudi za Kwara Falcons.

“Nawasifu Falcons kwa kuonyesha mchezo mzuri” alisema.

Lakini Filer, ambaye yuko katika msimu wa pili wa BAL, aliendelea kueleza kuwa "ushindi unaofuata siku zote ni ushindi bora zaidi."

XS
SM
MD
LG