Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Burkina Faso katika miaka ya karibuni imeshuhudia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwenye vikosi vyake vya usalama wakati ikiendelea kukabiliana na makundi ya wanamgambo kama vile al Qaida na Islamic State.
Ziara yake hiyo ya siku nne imempeleka kwenye eneo lililoathiriwa zaidi la Sahel, wakati akizungumza na baadhi ya viongozi akiwemo rais Roch Marc Christian Kabore, viongozi wa kidini, asasi za kiraia pamoja na baadhi waathirika.
Ziara ya Bachelet imefanyika wakati kukiwa na ongezeko la visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa maafisa wa usalama pamoja na wanamgambo katika wiki za karibuni. Wiki iliopita, takriban watu 15 wanasemekana kuuwawa na jeshi la serikali kwenye eneo la kusini magharibi mwa taifa, kulingana na asasi za kiraia.