Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 10:21

Baada ya mgogoro wa Tigray, raia wa Ethiopia wakabiliwa na tatizo la chakula


Wakati wa Ethiopia wakiachana na kipindi cha miaka miwili ya mgogoro, utafiti mpya wa Gallup unatoa picha kamili ya namna watu wanavyo taabika kiuchumi na msongo wa mawazo.

Utafiti umefanyika mwishoni mwa mwaka 2022, na kukuta kiwango kikubwa cha asilimia 65 ya Wa-Ethiopia wanataabika na kuhimili kupata chakula, ambapo bei za vyakula imepanda kwa asilimia 43 mwaka 2022 ukilinganisha na 2021, huku bidhaa nyingine zikipanda kwa zaidi ya asilimia 80.

Watafiti hawakufanikiwa kuingia nchini humo kwa mwaka 2021, na kuona mabadiliko makubwa walipo rejea mwaka uliofuata.

Zack Bikus mkurugenzi wa ukanda wa Afrika wa taasisi ya Gallup, amesema timu yao iliwafanyia mahojiano takriban watu 1,000 lakini hawakufanikiwa kusafiri maeneo ya mgogoro kama vile mkoa wa kaskazini wa Tigray.

XS
SM
MD
LG