Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:31

AU yatafuta suluhu Libya


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisalimiana na Moammar Gadhafi .
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisalimiana na Moammar Gadhafi .

AU , baraza la mpito la waasi na wawakilishi wa Moammar Gadhafi wakutana kutafuta suluhu Libya.

Wawakilishi kutoka serikali ya Moammar Gadhafi na baraza la mpito la kitaifa la waasi wote wako kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Malabo ambako viongozi wa Afrika watawasilisha utaratibu wa kumaliza mzozo wa Libya.

Pendekezo hilo linaandikwa na marais watano wa Afrika, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mohammed Ould Abdel Aziz wa Mauritania, Yoweri Museveni wa Uganda, Amadou Toumani Toure wa Mali na Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Congo.

Pendekezo hilo linataka kuwepo kwa sitisho la mapigano na kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia. Serikali ya Gadhafi inaonekana kuukubali mpango huo, lakini waasi wanataka pendekezo lijumuishe madai kwamba kiongozi wa Libya ni vyema aachie madaraka haraka.

Wakati mzozo wa Libya unatarajiwa kutawala mkutano huo, kamishna wa umoja wa Afrika, Jean Ping anasema viongozi pia watalenga mada ya mkutano huo vijana maendeleo stahmilivu.


Ping amesema "hakuna amani bila ya maendeleo, hakuna maendeleo bila ya amani, amani, demokrasia na maendeleo vinakwenda sambamba".

XS
SM
MD
LG