Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:10

Athari za kusitishwa mradi wa ujenzi wa bomba la matufa Uganda


Head of the Middle East and North Africa division at Total, Stephane Michel, left, and managing director of the National Iranian Oil Company Ali Kardor, right, shake hands after signing documents in Tehran, Nov. 8, 2016.
Head of the Middle East and North Africa division at Total, Stephane Michel, left, and managing director of the National Iranian Oil Company Ali Kardor, right, shake hands after signing documents in Tehran, Nov. 8, 2016.

Wachambuzi wa biashara ya mafuta wanasema hatua ya Kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total, kujiondoa kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, itaathiri kwa kiasi kikubwa Uganda.

Total imeamua kuondoka kwenye usimamizi wa ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,445 baada ya kushindwa kuafikiana na kampuni ya Tullow juu ya uuzaji wa vitalu vya mafuta wiki iliopita. Tullow ilitaka pia kuiuzia vitalu hivyo kampuni ya CNOOC ya Uchina.

“Kuondoka kwa Total kwenye mradi huo, hakika itaathiri pande zote husika hasa serekali ya Uganda, kwa sababu mradi huo utacheleshwa hadi muda usiojulikana, anasema Joe Watson Gakuo, mchambuzi wa biashara ya mafuta kutoka Kenya. Ameongeza kuwa Kampuni za Total, Tullow na CNOOC ambazo tayari zina leseni ya kuchimba mafuta, nazo zitapata hasara bila kusahau wawekezaji na wafanyabiashara ambao wangenufaika na mradi huo.

Mradi wa ujenzi wa bomba hilo ungegharimu dola billioni 3.5, kutoka Hoima magharibi mwa Uganda hadi bahari ya Tanga, kaskazini mwa Tanzania.

Kiini cha usitishwaji wa ujenzi wa bomba hilo, ni utata kati ya serikali ya Uganda na Kampuni ya Tullow kuhusiana na malipo ya ushuru.

Watson Gakuo ameiambia Sauti ya Amerika kwamba kuna ulazima serekali ya Uganda iligeze msimamo wake katika kutoza ushuru.

“Uganda ingeacha tama ya kutaka pesa nyingi kwa haraka, huu ni mradi ambao utadumu muda mrefu na mapato yake yanakadiriwa kuwa ya ma billioni ya dola.”

Uganda iligundua mafuta ghafi mwaka wa 2006, lakini uchimbaji wa kibiashara ulicheleweshwa kutokana na ukosefu wa miundombinu, ikiwemo bomba la mafuta.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG