Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 01:58

Assange akiri kufanya kosa la jinai


Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange amekiri shtaka moja la jinai kwa kuchapisha taarifa za siri za kijeshi za Marekani katika makubaliano na waendesha mashtaka wa wizara ya sheria ya Marekani.

Hatua hiyo inamuhakikishia uhuru wake na kuhitimisha sakata la kisheria lililoibua maswali yenye mgawanyiko kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa taifa.

Ombi hilo liliingizwa Jumatano asubuhi katika mahakama ya shirikisho mjini Saipan, mji mkuu wa Visiwa vya Mariana Kaskazini, himaya ya Marekani katika Pasifiki.

Alifika mahakamani muda mfupi kabla ya shauri kuanza kusikilizwa na hakujibu maswali. Ingawa makubaliano na waendesha mashitaka yalimhitaji kukiri hatia kwa kosa moja la uhalifu, ingemruhusu pia kurudi katika nchi yake ya asili ya Australia bila kukaa muda wowote katika gereza la Marekani.

Alifungwa Uingereza kwa miaka mitano iliyopita, akipambana na kupelekwa Marekani kwa hati ya mashtaka ya Sheria ya Ujasusi.

Forum

XS
SM
MD
LG