Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:42

Asasi za kiraia: Watu 8 wapoteza maisha katika gereza kuu la mji wa Bukavu


Jela kuu ya mji wa Bukavu.
Jela kuu ya mji wa Bukavu.

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Asasi za kiraia zinaeleza kuwa watu 8 wamepoteza maisha katika gereza kuu la mji wa Bukavu kutokana na ukosefu wa chakula na huduma za afya.

Hata hivyo, mamlaka husika na wafungwa imesema chakula kipo ndani ya gereza hilo.

Katika taarifa kwa wanahabari, mfumo wa mashauriano wa asasi za kiraia Kivu kusini unasema ulifanya uchunguzi katika gereza hilo na kugundua hali ya kusikitisha.

Gereza hilo lilolotarajiwa kupokea wafungwa 500, sasa linawafungwa 2050 akiwa pia mwanasheria, Zozo Sakali ndiye msimamizi wa mfumo wa mashauriano wa asasi za kiraia jimboni Kivu kusini anaamini kuwa gereza kuu la Bukavu limegeuzwa kuwa mahali pa kifo.

“Kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 22 machi tumehesabu sasa wafungwa 8 wa kiume waliofariki, miongoni kuna wale waliokuwa bado kufanya masambo. Walifariki kwakukosa chakula, dawa, hawaku shughulikiwa na serikali imebaki kimya. Hili tukio limetusikitisha na hatutabaki tena kimya” alisema Zozo Sakali.

Hali ya wafungwa katika magereza ya jimbo la Kivu Kusini imezidi kuwa ya kusikitisha naya kutokubalika. Hospitali kuu ya Bukavu iliyopokea wagonjwa miongoni mwa wafungwa kwasasa inasita kwavile bili zimekuwa nyingi mno bila serikali kulipa.

Kwa hivyo, asasi za kiraia zinahisi kwamba ni muhimu mamlaka husika ichukuwe maamuzi ya haraka ili kupunguza vifo, njaa na magonjwa kwa wafungwa katika magereza ya kivu kusini.

Lakini msimamizi wa gereza kuu la Bukavu Ilunga Dilamuna ametupilia mbali madai yakuwa wafungwa hao wamefariki kutokana na ukosefu wa chakula akihakikisha kwamba chakula kipo gerezani. Ilunga Dilamuna anahisi kwamba kilicho sababisha wafungwa kufariki ni idadi yao iliyoongezeka kupita kiasi gerezani

“Hawajafanya hata siku moja bila kula. Ni magonjwa yaliyosababishwa na uwingi wa wafungwa gerezani. Ikiwa mtu ni mgonjwa anatakiwa kupelekwa hospitalini, na hapo tuna tatizo kwani hospitali haikubali tena wafungwa sababu bili zimeongezeka sana. Eti wafungwa walifariki kutokana na ulaji mbaya, si sahihi” aliongeza Ilunga Dilamuna.

Wakati wa ziara yake ya hivi karibuni jimboni Kivu kusini, naibu waziri wa Sheria nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Amato Bayubasire amesisitiza akisema "Hatuwezi kubali ndugu zetu njaa iwapate ndani ya jela, na ndio kwa maana napenda kujulisha kwamba kila miezi 3 chakula kinafikishwa”.

Mnamo mwezi January, msimamizi wa gereza la Kamituga alikamatwa kwa tuhuma za ufisadi na kufungwa kwa muda katika gereza hilo hilo nahivyo kuhonja mateso ya wafungwa.

Imeandaliwa na mwandishi wetu Mitima Delachance, Sauti ya Amerika, Bukavu.

XS
SM
MD
LG