Timu ya soka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita imetolewa kwa kuvuliwa nafasi iliyoipata ya kushiriki katika hatua ya makundi ya klabu bingwa barani afrika.
Shirikisho la kabumbu barani Afrika (CAF) limetangaza uamuzi huo Jumanne kupitia ujumbe wa Twitter kwamba nafasi ya timu hiyo itachukuliwa na timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Uamuzi huo ulitolewa na kamati ya mashindano ya shirikisho hilo iliyokutana Jumanne kupitia malalamik yaliyowasilishwa na timu ya Stade Malien ya Mali kuhusu mchezaji wao wa zamani Idrissa Traore.
Traore alichezea klabu hiyo ya Mali katika msimu uliopita ambapo kamati ya nidhamu ya CAF ilimfungia mchezaji huyo kutocheza michezo minne katika ligi hiyo ya barani humo.
AS Vita ilimchezesha mchezaji huyo akiwa bado anatumikia adhabu yake katika mechi ya marudiano baina ya Sundows, mechi iliyokwisha kwa AS Vita kuibuka na ushindi.
Timu ya Mamelodi Sundowns sasa itajumuishwa katika droo ya kupanga makundi katika hatua ya kuelekea robo fainali.