Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 19:40

ANC yasherehekea miaka 100 Afrika Kusini


Picha ya rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela katika mapambo ya maadhimisho ya miaka 100 ya chama cha ANC
Picha ya rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela katika mapambo ya maadhimisho ya miaka 100 ya chama cha ANC

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wahudhuria sherehe za ANC mjini Bloemfontein

Maelfu ya watu Jumapili walikusanyika katika uwanja wa mchezo wa raga katika mji wa Bloemfontein Afrika Kusini kusherehekea miaka mia moja ya chama tawala African National Congress- ANC.

Sherehe hizo ambazo zimehutubiwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma zimehitimisha sherehe mbalimbali za mwishoni mwa wiki kwa heshima ya chama kikongwe barani Afrika kilichokuwa chanzo cha kupigania ukombozi.

Saa sita usiku kuamkia Jumapili saa za Afrika Kusini rais Zuma aliwasha mwange katika kanisa la Bloemfontein ambapo wasomi weusi na wanaharakati walizindua chama hicho cha ANC Januari 8 mwaka wa 1912. Dazeni ya viongozi kutoka nchi nyingine za Afrika walihudhuria sherehe hizo kukitambua chama cha ANC ambacho kiliongozwa na rais mstaafu Nelson Mandela baada ya kutimuliwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Bwana Mandela hata hivyo hakuhudhuria sherehe hizo kwa sababu afya yake imedhoofika. Chama cha ANC kilianzishwa kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na hatimaye kupata ushindi mwaka wa 1994 kilipotimua utawala wa wazungu waliokuwa wachache huko Afrika Kusini. Nelson Mandela alikuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG