Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:32

Chama tawala Afrika Kusini chakutana kumteua mrithi wa Zuma


Wafuasi wa Jacob Zuma wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais ndani ya ANC huko Pretoria, Julai 05, 2016.
Wafuasi wa Jacob Zuma wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais ndani ya ANC huko Pretoria, Julai 05, 2016.

Mkutano Mkuu unafanyika Jumamosi nchini Afrika Kusini ambapo chama tawala cha ANC kinaendelea na harakati za kumteua kiongozi mpya kushika hatamu na matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili.

Chama hicho ambacho kimekuwa chini ya uongozi wa Rais Jacob Zuma kwa miaka kumi hadi sasa.

Lakini vyanzo vya habari nchini Afrika Kusini vimesema kuwa mwelekeo wa chama hicho tawala umekuwa ukiyumba na kupoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na mipasuko ya kisiasa ndani ya chama.

Hata hivyo duru za kisiasa zinaeleza kuwa pamoja na mvutano huo ANC imeendelea kuwa na umaarufu katika harakati za kisiasa kutokana na kuwepo kwao madarakani kwa zaidi ya miongo miwili.

Kwa mujibu wa ratiba ya ANC mkutano huo unawakutanisha wajumbe wapatao elfu tano katika jiji la Johannesburg.

Imeelezwa kuwa Rais Jacob Zuma anatarajiwa kuwahutubia wajumbe wanaohudhuria mkutano huo mkuu.

Taarifa ya ANC imesema kuwa wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.

Lakini vuta ni kuvute ipo katika hatua za kumchagua mrithi wa Rais Zuma, kama kiongozi wa chama.

Ushindani huo ni kati ya mkewe wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma aliyewahi kuwa waziri na pia kutumikia nafasi ya uwenyekiti wa umoja wa Afrika.

Duru za siasa zinasema kuwa kuna upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa.

XS
SM
MD
LG