Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:30

Al-Shabaab washambulia AMISOM huko Somalia


Kikosi cha wanajeshi wa AMISOM huko Somalia
Kikosi cha wanajeshi wa AMISOM huko Somalia

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamefanya mashambulizi yaliyopangwa kutokea kwa wakati mmoja kwenye makambi matano ya jeshi katika wilaya ya Lower Shabelle huko Somalia, walioshuhudia na maafisa wanasema.

Maafisa wa Somalia wanasema malori mawili yaliyobeba wahanga wa kujitolea yalijaa milipuko iliyoteguka kwenye kambi ya jeshi ya AMISOM huko Bula Marer, kilomita 110 kusini ya Mogadishu na moja ya miji mikubwa katika mji. Hii ilifuatiwa na shambulizi lililofanywa na Al- Shabaab kwenye kambi.

Muda mfupi baadae bomu lililotegwa kwenye basi dogo lilipiga kituo kingine cha AMISOM kilicho jirani na kijiji cha Golweyn. Wanamgambo wa Al-Shabaab pia walishambulia kituo cha tatu cha AMISOM kwa makombora huko Barawe.

Wanamgambo hao pia walifanya mashambulizi kwenye majengo mawili ya serikali ya Somalia huko Qoryoley na Mashallay. Naibu gavana wa wilaya ya Lower Shabelle, Ali Nur Muhamed aliiambia Sauti ya Amerika kwamba vikosi vya AMISOM na Somalia vimejibu mashambulizi hayo yote.

XS
SM
MD
LG