Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:03

Chifu wa Mandera auawa na 'al-Shabaab'


Wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia
Wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia

Watu wenye silaha ambao wanasadikiwa kuwa wapiganaji wa Al-Shabaab wameshambulia kijiji kilicho karibu na mji wa Mandera na kumuua Chifu wa eneo hilo kabla ya kuwateka askari wa Kenya wawili, maafisa wamesema.

Kikundi hicho cha majangili kilivamia eneo la Omar Jillo, kaunti ndogo ya Lafey, Mandera Mashariki, ambayo ni takriban kilometa 16 kutoka mji wa Mandera Jumatatu usiku.

Polisi na wananchi wamesema maharamia hao walimpiga risasi chifu huyo baada ya kuvamia nyumbani kwake saa nne usiku katika tukio hilo. Mratibu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki Mohamud Saleh amesema kuwa maafisa wawili wa KPR wametoweka baada ya tukio hilo.

“Hatujui kama maafisa hao wametekwa au wamejificha.

Maharamia hao walitupa risasi ovyo ambapo zilipelekea kuuawa kwa chifu huyo katika eneo la nyumba yake,” amesema.

Amesema kuwa washukiwa wa kikundi hicho cha majambazi walitorokea upande wa mpaka wa Somalia ambao uko kilometa saba kutoka hapo palipotokea tukio hilo. Saleh amesema chifu huyo alikuwa amekalia kiti hicho kwa muda wa mwaka mmoja.

Wananchi wa eneo hilo walisikia milio sita ya bunduki kabla ya Chifu huyo kugundulika kuwa ameumizwa vibaya sana.

Omar Jillo ni kati ya miji iliyoko katika eneo hilo ambayo inamarufuku ya kutoka nje usiku kucha kutokana na hatari ya magaidi wa al-Shabaab.

XS
SM
MD
LG