Marais wa Benin, Togo na Ghana wamshuhudia hafla ya kuapishwa kwa rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara iliyofanyika leo jumatatu.
Outtara ameapishwa kwa mhula wa tatu madarakani wkaati kuna mzozo wa kisiasa kuhusu hatua yake ya kugombea mhula mwingine madarakani.
Outtara alishinda uchaguzi huo mwezi uliopita, ambao ulisusiwa na wanasiasa wa upinzani.
Ametangaza kwamba atamteua waziri mkuu katika serikali yake, katika juhudi za kuleta maelewano na vyama vingine vya kisiasa.
Uteuzi huo utafanyika kabla ya uchaguzi wa bunge mapema mwaka ujao.
Ameahidi pia kuunda wizara ya umoja na maridhiano ya taifa ilikuunganisha taifa hilo ambalo limegawanyika kisiasa. Wizara hiyo itasimamia mazungumzo ya umoja wa kitaifa.
Amesema kwamba agenda yake katika uongozi wake wa mhula wa tatu madarakani itakuwa kuimarisha sekta za elimu, afya na kubuni nafasi za ajira, akiongezea kwamba chanjo dhidi ya virusi vya Corona itaanza kutolewa nchini humo kuanzia April mwaka ujao.