Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:04

Aliyekuwa mlinzi wa Kiiza Besigye, ambaye alizuiliwa katika gereza la kijeshi DRC kwa miaka 8 ameachiliwa huru


Aliyekuwa mlinzi wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Sam Muhumya baada ya kuachiliwa huru DRC
Aliyekuwa mlinzi wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Sam Muhumya baada ya kuachiliwa huru DRC

Mfuasi mkubwa wa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda Sam Mugumya, ambaye amekuwa akizuiliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa muda wa miaka 8, ameachiliwa huru.

Mugumya amekuwa akizuiliwa katika gereza la kijeshi la Ndolo, tangu mwaka 2014.

Kulingana na mwanaharakati wa kisiasa nchini Uganda Dkt. Kiiza Besigye, Mugumya yupo huru.

“Mipango inaendelea kupitia kwa ubalozi wa Uganda mjini Kinshasa kuhakikisha kwamba Mugumya anapata stakabadhi za kusafiria ili arudi nyumbani. Watu wengine wanne wanaendelea kuzuiliwa,” ameandika Besigye kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kulingana na aliyekuwa msemaji wa jeshi la Uganda UPDF, Paddy Ankunda, Mugumya na watu wengine wanne raia wa Uganda, walikutwa na kiasi kikubwa cha pesa na nyaraka zinazowahusisha na kundi la waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliokuwa na nia ya kuupindua utawala wa rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Amekuwa akizuiliwa katika gereza la kijeshi la Ndolo, mjini Kinshasa.

Muguya aliandika barua kwa waziri wa sheria wa DRC mnamo mwaka 2017, akiomba “wamuue ilia pate uhuru wa daima.”

Alitoroka Uganda wakati maafisa wa usalama wa Uganda walikuwa wanafanya msako dhidi ya wanachama wa ngazi ya juu wa chama kikuu cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya kutaka kuipindua serikali ya rais Yoweri Museveni.

Dk Kiiza Besigye alisema kwamba “kukamatwa kwa Mugumya ilikuwa sehemu ya mpango mpana wa kutaka kuwakamata viongozi wa chama cha FDC na kuwahusisha na ugaidi ili kumzuia kugombea urais mwaka 2016.”

Haijabainika mazingira ambayo yamepelekea kuachiliwa huru kwa Mugumya na viongozi wa chama cha FDC hawajatoa taarifa zaidi kando na kutangaza kuachiliwa kwake.

Wamezuiliwa gerezani bila kushitakiwa, na serikali ya Uganda ilionekana kutotaka kuingilia kesi hiyo licha ya juhudi za makundi ya kisiasa na kutetea haki za kibinadamu.

“Tulijaribu kupata taarifa kutoka kwa serikali yetu bila mafanikio. Maafisa wa serikali ya Uganda wamekuwa wakituelekeza kwa ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,” wamekuwa wakisema watetezi wa haki za kibinadamu na wanasiasa wa upinzani nchini Uganda.

Raia wengine wa Uganda ambao wamekuwa wakizuiliwa pamoja na Mugumya ni Stephen Mugisha, Aggrey Kamukama, Joseph Kamugisha na Nathan Bright.

XS
SM
MD
LG