Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 17:12

Aliyekuwa Katibu mkuu wa EAC anatarajiwa kuhojiwa na Kamati  ya sheria, haki, na hadhi ya bunge la Jumuiya hiyo


Dr.Peter Mathuki aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akihojiwa na waandishi wa habari anatarajiwa kuhojiwa na Kamati  ya sheria, Haki, na Hadhi ya bunge la Jumuiya hiyo.
Dr.Peter Mathuki aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akihojiwa na waandishi wa habari anatarajiwa kuhojiwa na Kamati  ya sheria, Haki, na Hadhi ya bunge la Jumuiya hiyo.

Aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki  anatarajiwa kuhojiwa na Kamati  ya sheria, Haki, na Hadhi ya Bunge la Jumuiya  hiyo juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka,ofisi na mali za Jumuiya.

Dr. Mathuki ambaye aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo mwezi Mei 2021 na serikali ya nchi yake ya Kenya alitenguliwa na kupangiwa kazi nyingne na rais wa nchi hiyo mwezi Aprili mwaka 2024 baada ya baadhi ya wabunge kuwasilisha tuhuma zake katika kikao cha bunge hilo kilichokuwa kimekaa Nairobi Kenya.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Dr. Mathuki ni zile zinazohusishwa na matumizi mabaya ya ofisi, madaraka na mali za Jumuiya hiyo, tuhuma ambazo sasa zimefikishwa rasmi kwenye kamati ya sheria, haki na hadhi ya bunge hilo ambayo mwenyekiti wake Bw. Mashaka Ngole kutoka Tanzania amesema imeanza kuzifanyia kazi.

"Leo kama kamati tumekutana kwa lengo la kupata picha halisi kwamba hizo tuhuma uthibitisho wake uko wapi na kamati imepokea tuhuma kama zilivyowasilishwa na mpaka sasa hivi kamati haiwezi kusema lolote lakini tuhuma ni nyingi na ukizitazama zinazungumzia matumizi mabaya ya ofisi, masuala ya fedha, mambo ya uajiri ni mambo mengi yametajwa ambayo yanatuhitaji kutumia muda mwingi kuyapitia kwa kina.

Kwa mujibu wa Bw.Ngole katika utekelezaji wa majukumu hayo kamati inatarajia kuwashirikisha watu wote waliotajwa kushiriki katika mtandao huo akiwemo Mtuhumiwa mwenyewe Dr. Mathuki

Kwa kuwa ofisi zote zilizotajwa zina watu kamati italazimika kuwaita na kuwasikiliza juu ya hayo mambo yote yaliyotajwa kufanyika kwenye ofisi zao kwa hiyo wao ndio watatusaidia kutupatia ukweli halisi lakini tukimaliza hilo tutamuita pia mtuhumiwa Dr. Mathuki ili naye tumsikie.

Tuhuma dhidi ya katibu mkuu huyo ziliibuliwa na mbunge wa bunge hilo kutoka Sudan kusini Bw Kenned Mukulia ambaye pia ni amesema tatizo ni kubwa zaidi ya linavyoonekana na kwamba upo mtandao mkubwa na Ushahidi upo kwenye ripoti iliyowasilishwa kwenye kamati

Hili sio suala la katibu mkuu peke yake kuna watu wengine wengi wameshiriki kuwezesha na kufanikisha haya mambo yaani ni mtandao mkubwa

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kamati hiyo pamoja na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ofisi na mali za Jumuiya Dr. Mathuki ambaye kwa sasa serikali ya Kenya imemteua kuwa balozi pia anatuhumiwa kukiuka sheria za ajira za wafanyakazi na kwamba kamati hiyo baada ya kumaliza kazi yake itakabidhi ripoti kwenye Bunge la Jumuiya hiyo.

Licha ya baada ya Rais wa Kenya William Rutto kumuondoa Dr. Mathuki na kuteua Katibu mkuu mwingine hadi sasa bado hajaanza kazi na pia hajathibitishwa na ngazi zinazohusika ikiwemo ya wakuu wa nchi kama taratibu zinavyoelekeza.

Imeandaliwa na mwandishi wetu Asiraji Mvungi.

Forum

XS
SM
MD
LG