Kundi la waasi wa Somalia la Al Shabab limeapa kufanya vita vitakatifu dhidi ya kundi lolote la kulinda amani ambalo litaenda kusaidia serikali ya Somalia.
Al Shabab walifanya mikutano huko Beledweyne na miji mingine mitatu leo ambapo wazungumzaji walishutumu nchi za Afrika mashariki ambazo zimeahidi kupeleka majeshi ya ziada 2000 huko Somalia.
Mashahidi wanasema wanamgambo walikwenda nyumba hadi nyumba na kulazimisha watu waende kwenye mikutano hiyo.