Treni hizo mbili ziligongana karibu na jiji la Tempe, takriban kilomita 380 kaskazini mwa Athens, mji mkuu wa Ugiliki . Treni hiyo ya abiria ilikuwa ikielekea kaskazini ikitokea Athens kwenda katika jiji la Thessaloniki, wakati treni ya mizigo ilikuwa ikielekea kusini ikitokea eneo la Thessaloniki kwenda katika jiji la Larissa. Katika ajali hiyo mabehewa matatu ya abiria yaliacha njia na kuwaka moto.
Mamlaka zinasema kiasi cha abiria 250 ambao walinusurika kwenye ajali hiyo, au kupata majeraha madogo walisafirishwa kwa basi kwenda Thessaloniki. Treni ya abiria ilikuwa imebeba watu 350.
Inaelezewa wafanyakazi wa zima moto 150 wakiwa na magari 17 pamoja na magari ya kubeba wagonjwa 40 walifika katika eneo la maafa kutafuta abiria wengine ambao huenda bado wamebanwa na mabaki ya treni.
Kikosi cha huduma ya Zimamoto nchini Ugiriki imesema watu 66 wamelazwa hospitali, wakiwemo watu sita ambao wamewekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Msemaji wa Kikosi cha Zimamoto Vassilis Varthakogiannis alikiambia kituo cha television cha serikali kuwa juhudi za uokoaji zinafanyika “ katika mazingira magumu yaliyosababishwa na ukubwa wa ajali ya hizo za treni mbili.”